JESHI LA POLISI KATAVI LASISITIZA KUTUNZA SIRI ZA RAIA WEMA KUPAMBANA NA UHARIFU

Na.Issack Gerald-KATAVI
JESHI la Polisi Mkoani Katavi limesema linaendelea na utaratibu wa kutunza siri za raia wema wanaoshirikiana na Polisi kuwafichua waharifu wanaopelekea kusababisha madhara kwa wananchi.

Hayo yameelezwa leo na Afisa mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoani Katavi Focus Malengo wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu ushirikiano kati ya jeshi la polisi na raia katika juhudi za  kupambana na uharifu.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi kata,na viongozi wa kata na vijiji ili kuzuia uharifu kabla ya kutokea.
Miongoni mwa uharifu ambao umekuwa ukitajwa mara kwa mara kutokea Mkoani Katavi ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA