JAMII KATAVI,KIGOMA YATAKIWA KUWA NA UTAWALA BORA MATUMIZI YA RASILIMALI


Na.Issack Gerald-Katavi
Jamii katika mikoa ya Katavi na Kigoma imetakiwa kutumia sera ya utawala bora kutunza vyanzo vya rasilimali katika mazingira yanayoizunguka kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Wito huo umetolewa leo na Kaimu mkurugenzi wa Mpango wa kuhifadhi hifadhi  za Gombe,Masilo na Ugala Mary Mavanza katika kikao cha semina cha utawala bora katika Rasilimali ambacho kimefanyika Mjini Mpanda kikiratibiwa na taasisi ya Jane Goodal inayojishughulisha na uhifadhi wa mazingira hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi wa kuhifadhi mazingira wa taasisi ya Jane Goodal Mkoani Kigoma Emmanuel  Mtiti ameshauri elimu ya utawala bora wa rasilimali na utunzaji wa mazinginra kutolewa kuanzia ngazi ya mitaa.
Kikao hicho ambacho kimeanza leo mjini Mpanda kikiwashirikisha wataalamu wa masuala ya rasilimali na mazingira kutoka Wilayani Mpanda,Nsimbo,Uvinza na Kigoma kinatarajiwa kufikia tamati Ijumaa ya wiki hii.
Nao wajumbe walioshiriliki katika semina hiyo wamelisema kuwa viongozi wote wa umma wakiwemo wakurugenzi,wakuu wa wilaya na viongozi wa dini wanatakiwa kushirikishwa katika usimamizi wa rasilimali na utuunzaji wa mazingira ili wasaidie kueneza elimu ya mazingira kwa kiasi kikubwa.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA