Posts

Showing posts from February, 2018

MAJAMBAZI WAUA,WAJERUHI NA KUPORA MALI MGODINI MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwa rasasi   sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuvamiwa na majambazi   usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo uliopo Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi. Pamoja na kuwataja majeruhi,kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Jaffari Gwiyama Kitambwa,amemtaja aliyefariki kuwa ni Kalister Kalyalya(21) mkazi wa kata ya machimboni Wilayani Mpanda aliyepigwa risasi mgongoni na kutokezea tumboni.

MFAHAMU RAIS JACOB ZUMA AMBAYE AMEJIUZULU URAIS

Image
  Jacob Gedleyihlekisa Zuma   alizaliwa  Aprili 12, 1942 . Ni Rais wa  Afrika Kusini  tangu 2009.Alikuwa makamu wa rais chini ya  Thabo Mbeki  kati ya 1999 na 2005.Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha  ANC . KIJANA NA MWANAHARAKATI WA ANC Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la  Kwa Zulu-Natal .Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya  apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria). Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko  Robben Island  pamoja na  Nelson Mandela ambapo baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko  Msumbiji  na  Zambia na aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC. KUPANDA NGAZI KATIKA AFRIKA KUSINI HURU Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990,Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha ...

HATIMAYE RAIS ZUMA AJIUZULU

Image
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameamua kujiuzulu mara moja kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa chama chake kinachotawala nchini humo cha African National Congress, ANC. Chama tawala nchini Africa kusini cha ANC,kimepokea tangazo la kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma katika nafasi yake ya Urais. Afisa mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Ameongeza kwa kusema kuwa ANC haisherehekei hatua hiyo,kutokana na kuwa Zuma amekitumikia chama hicho kwa miaka 60. Awali kupitia televisheni Bw.Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo zingechafua jina lake. Makamu wa Rais wa Africa kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo. Zuma alikilalamikia chama cha ANC kwa kumtaka aondoke madarakani,ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya...

BARAZA LA MADIWANI LACHARUKA UPIGAJI CHAPA MIFUGO CHINI YA KIWANGO

Image
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida limewajia juu wataalamu wake kwa kutotekeleza kwa weledi upigaji chapa mifugo na kuwatishia kuwa watalamika kwenda kurudia zoezi hilo kwa gharama zao iwapo alama zinazowekwa zitafutika baada ya muda mfupi.   Katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kilichofanyika Mjini Kiomboi, ajenda iliyochukua uzito mkubwa ni juu ya kufutika kwa alama zilizowekwa kwenye upigaji chapa mifugo na kuchelewa kwa malipo ya wananchi walioshiriki  kusaidia  utekelezaji wa zoezi hilo.  Afisa mifugo Wilaya ya Iramba Andrew Manyerere anasema kuwa ingawa zoezi hilo lilitekelezwa kwa kuzingatia sheria lakini kwa mifugo ambayo alama zake zimefutika watarudia  bila malipo. Hata hivyo uamuzi wa baraza la madiwani wa uliotolewa na Mwenyekiti wake Simion Tyosela ni kwa wataalamu kufanyakazi hiyo kwa weledi vinginevyo watarudia zoezi hilo kwa gharama zao. Zaidi ya shilingi milioni 16 zi...

RAIS JACOB ZUMA ASEMA HAONI SABABU YOYOTE YA KUJIUZULU

Image
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema hajafanya makosa na haoni sababu ya kujiuzulu. Bw.Zuma alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumtaka kujiuzulu vinginevyo atakabiliwa na kura isiokuwa na imani dhidi yake leo Alhamisi. Image caption Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amesema kuwa haoni sababu ya yeye kujiuzulu Rais huyo amekuwa chini ya shinikizo ya kujiuzulu huku kukiwa na madai mengi ya ufisadi lakini amesema ANC imeshindwa kuelezea ni kwa nini ametakiwa kujiuzulu. Bw.Zuma amesema yuko tayari kuondoka baada ya mwezi Juni lakini akapinga vile jambo hilo linavyoangaziwa kwa sasa na alisema atatoa taarifa nyengine baadaye siku ya Jumatano. Chama cha ANC kimesema kilisikiza matamshi ya Bw.Zuma lakini kitatoa uamuzi wa hatua yake baadaye kabla ya kuzungumza. Kiongozi wa chama hicho Jackson Mthembu alitangaza kuwa kura isiokuwa na imani dhidi ya rais itasikilizwa siku ya Alhamisi huku Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi Disemba akiap...

MORGAN TSVANGIRAI AFARIKI DUNIA

Image
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini. Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC,Tsvangirai mwenye umri wa 65,na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo. Marehemu Morgan Tsvangirai Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri amesema marehemu alifariki jana jioni Februar 14. Katika kipindi cha uhai wake,maisha yake ya kazi yaligubikwa na harakati nyingi za kisiasa dhidi ya mpinzani wake Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe. Morgan Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000 na kuanza kutoa changamoto kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekaa madarakani muda mrefu. Kufuatia kifo hicho Bw.Tsvangirai,MDC inaelekea kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa. Bw.Tsvangirai,Ali...

RAIS MAGUFULI AMTEUA MNADHIMU WA JWTZ APANDISHA VYEO MABRIGEDIA 10 KUWA MAJENERALI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Rais wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli Pamoja na uteuzi huo,Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu ya Rais,Gerson Msigwa Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu. Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao; 1.                          Brig Jen. J.G. Kingu 2.                      ...

DC ACHARUKA WANANCHI KUTAPELIWA FEDHA ZA MASHINE ZA EFDs

Image
SERIKALI mkoani Katavi imetoa siku 14 kwa makampuni na wafanyabiashara waliochukua fedha kwa ajili ya kuwauzia mashine za EFDs wafanyabishara na mpaka sasa hawajui hatma ya fedha zao. Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lllian   Matinga alitoa siku hizo jana   katika kikao maalumu cha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa mkoa huo akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja jenerali   Mstaafu   Raphae Muhuga. Alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa makampuni yaliyokusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara na kuahidi kuwapelekea mashine za EFDs lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo.

AUAWA KWA KUKANYAGWA NA TEMBO

Image
MWANAMKE   aliyefahamika kwa jina la Maria Sekaye(60) mkazi wa kijijii cha Ilambila wilayani Kalambo   Mkoani Rukwa ameuawa baada ya kukanyagwa na tembo. Tembo hao wanaelezwa kuwa walikuwa njiani wakitokea katika pori la akiba la Lwafu mkoani Rukwa kuelekea katika nchi jirani ya Zambia. Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya Mkowe Alfred Mpandasharo alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 za asubuhi wakati mwanamke huyo akiwa ametoka kutembelea shamba lake lililokuwa limevamiwa na mazao kuliwa na tembo hao.

FAHAMU ASILI NA MAANA HALISI YA SIKU YA WAPENDANAO’’VALENTINE DAY’’

Image
Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi kwa Sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt.Valentine. Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa,ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi kwa sababu kwamba wakioa wasingekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga. Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele...

MPANDA RADIO YAONGOZA WANANCHI KATAVI KUSHEREHEKEA VALENTINE DAY KWA KUCHANGIA DAMU SALAMA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh.Salehe Mbwana Muhando,amekipongeza kituo cha matangazo cha Mpanda Radio kwa kuadhimisha siku ya wapendanao kwa kuwaunganisha Watanzania kwa kuchangia damu salama ili kunusuru wagonjwa. Akizindua kampeni hiyo ya uchangiaji damu salama iliyoandaliwa na kuratibiwa na Mpanda Radio Muhando ambaye amemwakilisha Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,amewataka Watanzania kuwa na moyo wa kujitolea katika mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo uchangiaji damu salama kwa ajili ya watu wenye uhitaji. Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mpanda Radio Bi.Salome Mchawa,amesema Mpanda Radio kama radio ya kijamii itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kujali mahitaji ya jamii huku akiwashukuru na kupongeza watanzania kwa kuunga mkono kampeni ya uchangiaji damu salama iliyoanzishwa na Mpanda Radio kama kushrehekea siku ya wapendanao’’ Valentine Day’’. Kituo cha Matangazo cha Mpanda Radio Fm kilichoanzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na mwenge wa...

CHAMA CHA ANC CHAAMUA ZUMA NI LAZIMA AONDOKE

Image
Chama tawala Afrika kusini African National Congress (ANC) kimemuomba rasmi rais Jacob Zuma ajiuzulu baada ya yeye kukataa kufanya hivyo mapema hii leo. Taarifa kuhusu uamuzi huo umefuata mfululizo wa mazungumzo ya maafisa wa juu wa chama hicho yalioendelea usiku kucha hadi kuamkia alfajiri ya leo. Haki miliki ya picha Muhula wa Zuma unamalizika mwaka ujao Iwapo Bw.Zuma(75) hatoteteleka atakabiliwana na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni ambayo anatarajiwa kushindwa. Akiwa amehudumu madarakani tangu 2009, ameandamwa kwa tuhuma za rushwa. Haki miliki ya picha Imebainika kuwa mrithi wake Zuma atakuwa Cyril Ramaphosa kwasababu ndiye rais wa chama cha ANC. Chama cha ANC hakijathibitisha rasmi mipango yake lakini duru kutoka cham hicho zimetoa ufafanuzi katika vyombo vya habari nchini Afrika kusini na pia kwa shirika la habara la kimataifa la Reuters. Rais Zuma amekiuka shinikizo linaloongezeka la kumtaka ajiuzulu tangu Desemba wakati Cyril Ramaphosa alipoichukua nafa...

MWANASHERIA MKUU WA KENYA PROFESA GITHU MUIGAI ABWAGA MANYANGA

Image
Mwanasheria mkuu wa Kenya Profesa Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita na nusu ambapo kufuatia uamuzi huo Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa huduma zake na sasa jaji Paul Kihara Kariuki atachukua mahala pake. Kabla ya uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu profesa Muigai alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya mawakili ya Mohammed Muigai na amekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi. Haki miliki ya picha Mwanasheria mkuu wa Kenya Professa Githu Muigai Aidha alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha sheria cha Columbia mjini New York ambapo Kutoka 1984 alikuwa mwanfunzi katika chuo cha kusomea uanasheria nchini Kenya . Wakati huo huo alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi huku akiwa mshauri wa serikali katika maswala ya kisheria, Githu Muiga atakumbukwa kwa kuleta sheria za mageuzi katika timu ya uchaguzi nchini Kenya siku chache tu kabla ya uchaguzi kufanyika. Katika sheria hiyo kamishna yeyote yul...

WANAFUNZI WA SEKONDARI WASOMEA KATIKA VYUMBA VYA MAABALA

Image
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kasokola iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wanalazimika kusomea katika vyumba vya maabala vyenye kemikali za kisayansi zinazotumika kwa ajili ya masomo ya fikizikia,Kemia na baiolojia. Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameiomba serikali na wadau kujenga vyumba vya madarasa ili kuwaepusha na mazingira hatarishi walimu na wanafunzi. Kwa upande wake Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Kasokola Joel Mwandwanda amesema wanafunzi kusomea katika vyumba vya maabala kunatokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo ambapo hata walimu wamegeuza maabala hizo na baadhi ya vyumba vya madarasa kuwa ofisi.

ANC CHAADHIMISHA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWA NELSON MANDELA

Image
Chama tawala cha Africa Kusini ANC kimeanza maadhimisho ya kumbukumbu za miaka mia moja tangu kuzaliwa kwa Raisi wa kwanza mweusi nchini humo shujaa Nelson mandela. Nelson Mandela Kiongozi wa sasa wa ANC ,Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutoa hotuba huko medani mwa Freedom square mjini Cape Town, ambako marehemu Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza alipoachilia huru kutoka gerezani miaka ishirini na nane iliyopita.

DR. SHEIN AAGIZA WIZARA YA ELIMU KULIPA MADENI YOTE YA WALIMU KABLA 2019

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein amesema sera ya elimu bure  kwa wanafunzi wa sekondari itaanza ifikapo  mwezi june  mwaka huu. Akizungumza  katika Mkutano Mkuu wa Sita wa chama cha walimu Zanzibar zatu amesema serikali imeamua  kuondoa ada  kwa wanafunzi  kwa lengo la kuendeleza sera ya rais wa awamu ya kwanza Shekh Abeid Amani Karume.

RAIS MAGUFULI AMPANDISHA CHEO NA KUMTEUA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amempandisha cheo na kumteua Bw.Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Taarifa ambayo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw.Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP)na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo Februari 10 ambapo kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar. Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

TANZANIA YARIDHIA KUFUTA TOZO YA DOLA ZA KIMAREKANI

Image
Tanzania imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 inayotozwa kwa kila stika katika magari yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi. Hatua hii imefikiwa katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umeafnyika Jijini Arusha Akizungumza katika Mkutano huo,Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage amesema Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla. Tozo hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi. Mkutano huu uliofanyika Februari 7 mpaka 9 mwaka huu pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ambavyo vimekuwepo kwa muda mrefu katika Jumuiya. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA MAAMUZI YA UN

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuanza kutekeleza sera ya kupunguza gharama kwenye misheni za kulinda amani. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaziwakilisha nchi zao hapa nchini mkutano ambao umefanyika ikulu jijini Dar es salaam. Amesema hatua hiyo itadhohofisha jitihada za kutafuta amani kwenye maeneo yenye migogoro na kuhatarisha maisha ya walinda amani pamoja na raia wasio na hatia wanaoishi kwenye maeneo yenye migogoro. Wakati huo huo pamoja na mambo mengine Mhe.Rais Magufuli amesema pamoja na nia njema ya mpango wa majaribio wa kutafuta suluhu la kudumu ya tatizo la wakimbizi,Tanzania imeamua kujitoa kutokana na changamoto za kiusalama na ukosefu wa fedha za kugharamia mpango huo. Wakati huo Rais Magufuli amesema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wakiwemo wa kimataifa wote wanaohitaji kuwekeza hap...