MWANASHERIA MKUU WA KENYA PROFESA GITHU MUIGAI ABWAGA MANYANGA
Mwanasheria mkuu wa Kenya Profesa
Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita na nusu ambapo
kufuatia uamuzi huo Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa huduma
zake na sasa jaji Paul Kihara Kariuki atachukua mahala pake.
Kabla ya uteuzi wake kuwa mwanasheria
mkuu profesa Muigai alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya mawakili ya
Mohammed Muigai na amekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana
na ubaguzi wa rangi.
Aidha alikuwa mwanafunzi katika chuo
kikuu cha sheria cha Columbia mjini New York ambapo Kutoka 1984 alikuwa
mwanfunzi katika chuo cha kusomea uanasheria nchini Kenya .
Wakati huo huo alikuwa mwanafunzi wa
chuo kikuu cha Nairobi huku akiwa mshauri wa serikali katika maswala ya
kisheria, Githu Muiga atakumbukwa kwa kuleta sheria za mageuzi katika timu ya
uchaguzi nchini Kenya siku chache tu kabla ya uchaguzi kufanyika.
Katika sheria hiyo kamishna yeyote
yule katika tume ya uchaguzi alipewa nguvu za kumtangaza mshindi wa uchaguzi
iwapo mwenyekiti wa tume hiyo hayupo.
Sheria hiyo ilizua pingamizi kutoka
kwa upinzani pamoja na jamii ya kitaifa waliodai kuwa serikali haiwezi kufanya
mabadiliko ya sheria za uchaguzi wakati ambapo uchaguzi mkuu unakaribia.
Katika hatua nyingine Githu Muigai
atakumbukwa katika hatua ya
kuliharamisha kundi la upinzani la NRM hatua ambayo pia ilipingwa na viongozi
wa upinzani wakisema kuwa ni hatua mojawapo ya serikali ya kutaka kukandamiza
upinzani.
Siku chache kabla ya kiongozi wa
upinzani Raila Odinga aliyejiita kuwa 'rais wa wananchi' kula kiapo,Bwana Githu
alitishia kuwa mtu atakayejaribu kula kipao cha urais atajilaumu mwenyewe kwa
kuwa mashtaka yatakayomkabili ni ya uhaini ambao hukumu yake ni mtu kunyongwa.
Hatahivyo Raila alikula kiapo hicho
katika bustani ya Uhuru Park katika hafla iliohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa
upinzani na matokeo yake yalisababisha viongozi wa karibu walioshiriki katika
kumlisha bwana Raila Kiapo hicho kukamatwa na kushatkiwa huku wengine
wakifurushwa kutoka nchini.
Hatahivyo viongozi wengine wakuu wa
upinzani hawakuhudhuria hafla hiyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments