CHAMA CHA ANC CHAAMUA ZUMA NI LAZIMA AONDOKE
Chama tawala Afrika kusini African
National Congress (ANC) kimemuomba rasmi rais Jacob Zuma ajiuzulu baada ya yeye
kukataa kufanya hivyo mapema hii leo.
Taarifa kuhusu uamuzi huo umefuata
mfululizo wa mazungumzo ya maafisa wa juu wa chama hicho yalioendelea usiku
kucha hadi kuamkia alfajiri ya leo.
Iwapo Bw.Zuma(75) hatoteteleka atakabiliwana
na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni ambayo anatarajiwa kushindwa.
Akiwa amehudumu madarakani tangu
2009, ameandamwa kwa tuhuma za rushwa.
Chama cha ANC hakijathibitisha rasmi
mipango yake lakini duru kutoka cham hicho zimetoa ufafanuzi katika vyombo vya
habari nchini Afrika kusini na pia kwa shirika la habara la kimataifa la
Reuters.
Rais Zuma amekiuka shinikizo
linaloongezeka la kumtaka ajiuzulu tangu Desemba wakati Cyril Ramaphosa
alipoichukua nafasi yake kama kiongozi wa chama cha ANC.
Katibu mkuu wa ANC Ace Magashule
ameiwasilisha barua kwa kiongozi huyo anayepigwa vita nyumbani kwake katika mji
mkuu Pretoria na kumuarifu rasmi kuhusu uamuzi wa chama hicho wa kumtaka
aondoke katika mkutano na kamati ya kitaifa ya utendaji (NEC), taarifa
zinasema.
Kimsingi rais Zuma amekubali kuondoka
lakini anataka muda wa ilani wa kati ya miezi 3 na 6.
Hakujatolewa muda wa mwisho kwake
kuondoka madarakani, lakini imebainika kuwa mrithi wake atakuwa Cyril Ramaphosa
kwasababu ndiye rais wa chama cha ANC.
Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia
rahisi zaidi ya chama hicho kumng'oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri
utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama
cha ANC.
Rais Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na
mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa uongozi wa chama tawala Desemba mwaka
jana.
Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa
anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye
kushika pia nafasi hiyo.
Ramaphosa ameahidi pia kupambana na
rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea
katika uchaguzi mwakani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments