WANAFUNZI WA SEKONDARI WASOMEA KATIKA VYUMBA VYA MAABALA
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Kasokola iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wanalazimika kusomea katika
vyumba vya maabala vyenye kemikali za kisayansi zinazotumika kwa ajili ya
masomo ya fikizikia,Kemia na baiolojia.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameiomba serikali na wadau kujenga vyumba
vya madarasa ili kuwaepusha na mazingira hatarishi walimu na wanafunzi.
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa shule
ya sekondari Kasokola Joel Mwandwanda amesema wanafunzi kusomea katika vyumba
vya maabala kunatokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo ambapo
hata walimu wamegeuza maabala hizo na baadhi ya vyumba vya madarasa kuwa ofisi.
Kwa mjibu wa kaimu Mkuu wa shule hiyo
yenye wanafunzi 415 iliyoanzishwa tangu mwaka 2008 ina upungufu wa walimu hasa katika
masomo ya Sayansi ambapo kwa sasa kuna walimu wawili mmoja akifundisha
hisababti na mwingine Kemia kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Shule hiyo tangu mwaka 2008
ilipoanzishwa mpaka kufikia mwaka 2016 haikuwa na mwalimu wa sayansi hata mmoja
suala ambalo lilikuwa gumu kwa wanafunzi hasa wanaofanya mitihani kwa vitendo
katika masomo ya Fizikia,Kemia na Baiolojia kushindwa kufaulu vizuri.
Pia kaimu Mkuu wa shule hiyo amebainisha
changamoto nyingine ambazo ni kikwazo kwa shule hiyo kuwa ni uahaba wa walimu
wa sayansi,uhaba wa vyumba vya madarasa na kusababisha wanafunzi zaidi ya
wastani unaotakiwa kuwa katika chumba kimoja.
Hata hivyo licha ya changamoto
hizo,shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika mtiohani wa kidato cha nne.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments