ANC CHAADHIMISHA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWA NELSON MANDELA
Chama tawala cha Africa Kusini ANC
kimeanza maadhimisho ya kumbukumbu za miaka mia moja tangu kuzaliwa kwa Raisi
wa kwanza mweusi nchini humo shujaa Nelson mandela.
Kiongozi wa sasa wa ANC ,Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutoa
hotuba huko medani mwa Freedom square mjini Cape Town, ambako marehemu Mandela
alitoa hotuba yake ya kwanza alipoachilia huru kutoka gerezani miaka ishirini
na nane iliyopita.
Rais Jacob Zuma ambae anakabiliwa na madai chungu nzima ya
rushwa amegoma kubanduka huku shinikizo za kumtaka ajiuzulu zikizidi kumzonga .
ANC imetangaza mkutano maalum wa kamati yake kuu ya kitaifa
utafanyika Jumatatu kujadili swala hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments