DR. SHEIN AAGIZA WIZARA YA ELIMU KULIPA MADENI YOTE YA WALIMU KABLA 2019
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohammed
Shein amesema sera ya elimu bure kwa wanafunzi wa sekondari itaanza
ifikapo mwezi june mwaka huu.
Akizungumza katika
Mkutano Mkuu wa Sita wa chama cha walimu Zanzibar zatu amesema serikali
imeamua kuondoa ada kwa wanafunzi kwa lengo la
kuendeleza sera ya rais wa awamu ya kwanza Shekh Abeid Amani Karume.
Amesema sera
ya elimu bure itaimarika endapo walimu watafanya kazi kwa mujibu wa sheria na
maendeleo ya elimu yatajengeka iwapo walimu watakuwa na
juhudi na uimara pamoja na misingi bora na zamira njema
ya kufundisha wanafunzi maskulini.
Dr.shein
amesema anatambua matatizo yanayowakabili walimu pamoja na skuli
kukabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo uhaba wa walimu,
uchache wa vifaa vya kufundishia pamoja na malimbikizo ya madeni ya mishahara
ya walimu na kuiagiza wizara ya elimu kuhakikisha wanawalipa madeni
yote wanayodaiwa na walimu kabla ya kufikia 2019 kwani
kuendelea deni hilo litaweza kuondoa ari ya walimu kufundisha na kupelekea
sekta ya elimu kuyumba kutokana na maslahi madogo ya walimu.
Hata
hivyo Rais Shein amesema amerizishwa na matokeo yaliyopatikana
katika mitihani ya taifa kwa elimu ya msingi na sekondari na kuitaka
wizara ya elimu kukaa pamoja na skuli zote za Zanzibar
zile zilizofanya vibaya katika mitihani ya taifa ili kuweza
kujua sababu zilizopelekea kufeli.
Aidha
amesema serikali itaendelea kujali na kuthamini michango ya
walimu yanayotoka katika taifa kwa kujali maslahi yao
kila uchumi wan chi utakavyo imarika.
Kwaupande
wake Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar zatu Mussa Omar Tafurwa Mapema
akisoma risala ya walimu amesema miongoni mwa matatizo yanayowakabili ni tatizo
la uhaba wa walimu kwa skuli za pemba na mikoa ya
kaskazini na kusini kwa unguja.
Tafurwa
ameiyomba serikali kufanya uwekezaji
wa rasilimali fedha ya kutosha ili kuweza kuajiri
walimu pamoja,kununulia vifaa vya kufundishia pamoja na kulipa
madeni ya walimu wanayodai kwani pia baadhi yao wamesha staafu na wengine
kufariki.
Amesema
pia licha ya matatizo hayo pia walimu wanakabiliwa na mazingira
magumu ya kufundishia ambapo hupelekea kuumwa na kushindwa kufanya kazi
vizuri hivyo wameiyomba serikali kuwaanzishia bima ya
afya kwani wanashindwa mukumu gharama za matibabu kwani
fedha wanayoipata bado haikidhi haja.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments