TANZANIA YARIDHIA KUFUTA TOZO YA DOLA ZA KIMAREKANI
Tanzania imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 inayotozwa kwa kila stika katika magari yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi.
Hatua
hii imefikiwa katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la
Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao
umeafnyika Jijini Arusha
Akizungumza
katika Mkutano huo,Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage
amesema Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea
kuboresha mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla.
Tozo
hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha
mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi.
Mkutano
huu uliofanyika Februari 7 mpaka 9 mwaka huu pamoja na mambo mengine ulilenga
kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ambavyo
vimekuwepo kwa muda mrefu katika Jumuiya.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments