MH.SUGU NA MASONGA WAACHIWA KWA DHAMANA HUKUMU YAO FEBRUARI 26,2018
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi''SUGU'' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.
Mh.Mbilinyi na Masonga ambao wameachiwa jana wamekuwa mahabusu kwa muda wa siku
24 baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande
wa Jamhuri.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite
amewaachia kwa dhamana wawili hao baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter
Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi
sita walitoa ushahidi wao.
Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kuwa Februari
19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo ambapo hakimu Mteite
amekubaliana na hoja hiyo ya mawakili na
kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.
Mh.Mbilinyi na Masonga wanakbiliwa na kesi ya kutumia
lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments