RAIS MAGUFULI AMPANDISHA CHEO NA KUMTEUA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amempandisha
cheo na kumteua Bw.Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Taarifa
ambayo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa
Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw.Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP)na kisha kumteua kuwa
Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Kamishna
wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa
Polisi Zanzibar kuanzia leo Februari 10 ambapo kabla ya uteuzi huu Kamishna wa
Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.
Kamishna
wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa
Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments