KIM JONG-UN AMUALIKA RAIS WA KOREA KUSINI
Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini
Kim Jong un amemualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kuzuru Pyongyang ambapo
Utakuwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja kati ya
viongozi hao wa Korea.
Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini |
Bw.Moon amesema Korea ni muhimu
kuhakikisha mkutano huo unafanyika huku akiitaka Korea Ksakzini kurudi katika
meza ya mazungumzo na Marekani.
Mualiko huo ulioandikwa ulikabidhiwa
kwa rais wa Korea Kusini na dadake rais Kim Jong un,Kim Yo Jong ambapo Katika
mkutano wa kihistoria uliofanyika katika jumba la rais kabla ya kuanza kwa
michezo hiyo ya msimu wa baridi.
Bi.Kim na kiongozi wa kisherehe wa
taifa la Korea Kaskazini Kim Yong-nam ndio viongozi wa ngazi za juu kutoka
Kaskazini kuzuru kusini tangu vita vya Korea 1950.
Rais Donald Trump na mwenzake wa Korea Kusini Kim Jae-in |
Wakati huohuo Rais wa Korea ya Kusini
Moon Jae amekuwa ni mwenye shughuli nyingi za kupokea ujumbe wa ngazi ya juu katika
ikulu yake ya mjini Seoul baada ya ufunguzi rasmi jana wa michezo ya Olympic ya
msimu wa baridi nchini humo ambapo jana amesalimiana na dada yake kiongozi wa
Korea kaskazini Kim Jong un.
Ulikuwa ni mara ya kwanza ujumbe kama
huo wa maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea
Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita ambapo hata hivyo
hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani.
Makamu rais wa Marekani,Mike Pence
alisusia mwaliko wa chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na
kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.
Taarifa kutoka chombo cha habari cha
Yo hap kimesema Pence alionana kidogo na bw.Kim wakati wakijaribu kukwepana
kuonana uso kwa uso.
Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo
kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambao unapingwa vikali
na majirani zake na vilevile Marekani.
Katika shughuli hiyo,Bw.Moon alisema
anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza
kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments