RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA MAAMUZI YA UN
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea
kusikitishwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuanza kutekeleza sera ya kupunguza
gharama kwenye misheni za kulinda amani.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na mabalozi na wakuu wa
mashirika ya kimataifa wanaziwakilisha nchi zao hapa nchini mkutano ambao
umefanyika ikulu jijini Dar es salaam.
Amesema
hatua hiyo itadhohofisha jitihada za kutafuta amani kwenye maeneo yenye
migogoro na kuhatarisha maisha ya walinda amani pamoja na raia wasio na hatia
wanaoishi kwenye maeneo yenye migogoro.
Wakati
huo huo pamoja na mambo mengine Mhe.Rais Magufuli amesema pamoja na nia njema
ya mpango wa majaribio wa kutafuta suluhu la kudumu ya tatizo la wakimbizi,Tanzania
imeamua kujitoa kutokana na changamoto za kiusalama na ukosefu wa fedha za
kugharamia mpango huo.
Wakati
huo Rais Magufuli amesema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wakiwemo
wa kimataifa wote wanaohitaji kuwekeza hapa nchini.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments