Posts

Showing posts from November, 2017

WAJUMBE CCM KATAVI:UCHAGUZI ULIKUWA NA DOSARI

Image
Na.Issack Gerald Baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi wamedai uchaguzi wa ndani kupitia jumuia za chama hicho kuwa na dosari. Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Kajoro Vyohoroka ambaye  ameeleza zoezi hilo kufanyika  vizuri huku akiongeza kusema kuwa anafuatilia katika jumuia zote ili kujua kama kulikua na changamoto zilizojitokeza. Uchaguzi wa kupata viongozi mbalimbali wa jumuia za chama cha Mapinduzi ulifanyika jana. Uchaguzi kama huo ndani ya chama cha Mpainduzi,umefanyika pia Zanzibar. Habari Zaidi NA P5TANZANIA LIMITED

LEO NI MAADHIMISHO SIKU YA MAULIDI

Image
Na.Issack Gerald Waisilamu wilayani Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wameombwa kuhudhuria maulidi ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Mtume Mohamadi yanayofanyika leo. Wito huo umetolewa na Shehe wa baraza kuu la waisilamu Tanzania BAKWATA Wilaya ya Mpanda  Iddi Shabani Kondo Wakati akizungumza na Mpanda Redio ambapo amewaomba waisilamu wote kudumisha amani kataika hadhara hiyo . Shehe Kondo amesema kuwa Maulidi hiyo itafanyika katika kata ya Stalike halmashauri ya nsimbo kuanzia saa 1:30 jioni. Amesema katika kuadhimisha siku hiyo waisilamu wote wanakumbuka kazi iliyofanywa na mtume Mohamadi ya kufikisha ujumbe rasmi wa mafundisho wa uisilamu. Maulidi hii ya mwaka 1439 wa dini ya kiisilamu sawa na mwaka 2017 kitaifa yatasomwa wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na tarehe 1/12 itakuwa ndio siku ya mapumziko. Habari Zaidi NA P5TANZANIA LIMITED

HALI YA TAHARUKI MKOANI RUKWA,JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU LIMETELEKEZWA

Image
Na.Issack Gerald Hali ya taharuki na hofu imezuka katika Kijiji cha Katani Kata ya Nkandasi wilayani Nkasi mkoani Rukwa na kusababisha waombolezaji kutimua mbio na kuacha jeneza lenye mwili wa marehemu baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha na kubomoa nyumba za wakazi wa kijiji hicho. Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kaungo, Robert Kanoni, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 6 mchana,  wakiwa wanaelekea kufanya maziko ya marehemu Dismas Kanoni aliyefariki jana baada ya kuugua siku chache zilizopita, ghafla ilianza kunyesha mvua kubwa ikiambatana na radi na upepo mkali ulioezua baadhi ya nyumba hali iliyosababisha baadhi ya waombolezaji kutimua mbio na kurejea majumbani kutokana na hofu iliyoibuka kufuatia tukio hilo. Baadhi ya wananchi walivumilia nakurejea na jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu nyumbani na kuahirisha maziko kwa muda ili kupisha hali hiyo itulie na walikwenda kuzika baadaye katika makaburi yaliyopo kijijini hapo. Alisema tukio hilo limezua hisia ...

WAKAZI MPANDA WANAISHI KWA HOFU YA USALAMA, WASHINDWA KUFANYA KAZI

Image
Na.Issack Gerald Wakazi wa vijiji vya Ndui Stesheni,Mnyaki A na Mnyaki B kata ya Katumba wilayani Mpanda Mkoani Katavi wanashindwa kufanya kazi za maendeleo kwa uhuru kutokana na uharifu unaofanywa na watu wasiojulikana. Hali hiyo imebainishwa na wakazi wa vijiji hivyo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti katika vijiji hivyo kutokana na matukio ya watu kuvamiwa nyumbani nyakati za usiku,kutekwa njiani na kuporwa mali. Wakazi wameliomba jeshi la polisi kuweka mkazo ili kutafuta namna ya kukomesha uharifu huo ambao umekuwa kero kwao. Mmoja wa viongozi katika maeneo hayo Bw.Hussein Nasri ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ndui Stesheni,amekiri kuwepo kwa matukio ya kiuharifu hasa unyang’anyi wa pikipiki matukio ambayo hivi karibuni yameripotiwa na wenyeviti wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B. Hivi karibuni,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda,akihojiwa na Mpanda Radio,alitoa kauli kuwa hajapokea za taarifa za kiuharifu za hivi karibuni hali ambay...

MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU AMEMJULIA HALI MH.TUNDU LISSU

Image
Na.Issack Gerald Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Mhe.Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake. Mhe.Tundu Lissu amemshukuru Mhe.Rais Magufuli na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao. Habari zaidi na P5TANZANIA LIMITED

RAIS KENYATTA AMEANZA SAFARI YA PILI MUHULA WA PILI WA URAIS

Image
Na.Issack Gerald Hatimaye jana Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kwa muhula wa pili wa miaka mitano katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Kasarani mwezi mmoja baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi uliosusiwa na mpinzani mkuu Raila Odinga. Kulikuwa na nderemo na shangwe katika uwanja huo kutoka kwa maelfu ya wananchi wengi wao wafuasi wa muungano wa chama tawala cha Jubilee waliojaa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani. Uwanja huo unaingiza watu 60,000 lakini habari zinasema walioingia walikuwa 100,000. Wageni waalikwa na watu mashuhuri wapatao 40 walihudhuria sherehe hizo wakiwemo zaidi ya viongozi wakuu wa nchi 10. Kenyatta,55,alishinda uchaguzi mkuu wa marudio wa Oktoba 26 kwa asilimia 98.Uchaguzi huo ulifanyika baada ya matokeo ya ushindi wa Agosti 8 kufutwa na Mahakama ya Juu kwa maombi ya Odinga aliyewasilisha ushahidi wa dosari na ukiukwaji wa katiba. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  ni miongoni viongo...

KASI YA KUMNASUA MTOTO WA KIKE HASA MIMBA ZA UTOTONI YAZIDI KUSHIKA KASI

Na.Issack Gerald WATOTO wa kike mkoani Rukwa wamepewa mafunzo maalumu ya namna ya kuzitambua changamoto mbalimbali zinazowakwamisha kuzitumia fursa zilizopo katika kutekeleza matarajio yao ili waweze kujitegemea. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi uitwao U-report unaotekelezwa na Tanzania Girl Guides Association mkufunzi wa mradi huo,Emiliana Stanslaus amesema wahitimu wapatao 20 katika kila halmashauri wamewezeshwa namna ya kuwasaidia wasichana wenzao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi yao. Amesema wasichana hao walipata mafunzo ya siku mbili ambapo watawasaidia wanafunzi wenzao wa kike katika shule za msingi na sekondari na wasichana waliopo vijijini katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kubakwa na pia kupata mimba za utotoni. Emiliana amesema mradi huo utatekelezwa katika halmashauri za Sumbawanga vijijini,Kalambo,Nkasi na Sumbawanga Manispaa kwa njia ya kutuma ujumbe wa maandishi ya simu kwenda namba maalumu ya 150...

RAIS MAGUFULI ASISITIZA JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA

Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe kwa sababu yeye ndiye rais kwa sasa tofauti na zamani alipokuwa waziri. Rais amesema hayo mapema leo wakati akihutubia wananchi ambao wamejitokeza katika ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila. Aidha rais Magufuli amesema Jengo hilo lazima libomolewe hata nusu ya jengo iliyopoo katika hifadhi ya barabara huku akisema na kama ni kuondoa jengo lote basi inamaanisha kuwa pia jengo la wizara ya maji nalo itabidhi liondolewe kwa kuwa sheria ni msumeno. Wakati huo huo rais amesema wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa fidia kwa sababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara na waliotakiwa kulipiwa fidia walikwishalipwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MKOA WA KATAVI UMEZINDUA SIKU 16 ZA KUPAMBA NA AKATIRI WA KIJINSIA

Na.Issack Gerald Mkoa wa Katavi umezindua siku 16 za kupinga ukatiri wa Kijnsia uzinduzi ambao umefanyika katika kata ya Kabungu wilayani Tanganyika ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 12 mwaka huu. Akizungumza katika uzinduzi huo,kamanda wa Polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amesema makosa ya ubakaji yamepungua kutoka matukio 100 kwa mwaka na kufikia matukio 68 kwa mwaka huu ambayo yameripotiwa. Aidha Kamanda Nyanda amewapongeza wananchi kwa kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kutoa taarifa mbalimbali ikiwepo za ukatili unaoendelea kutokea sehemu mbalimbali za mkoa huu. Kwa upande wao wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Katavi katika risala yao wameomba mkoa kutafuta njia za kupunguza au kumaliza tatizo la mimba za utotoni kwa kuwa ni miongoni mwa sababu inayosababisha vifo kwa watoto wengi kutokana na uzazi. Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa katavi Meja jenerali Rafaeli Muhuga mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wananchi kuacha kufuata mila potofu zi...

RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Mh.Uhuru Kenyatta. Taarifa ya serikali ambayo imetolewa na Mkurugenzi, Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi imethibitisha hilo. Mhe.Kenyatta anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo jijini Nairobi ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo. Rais Uhuru Kenyatta atakuwa anaongoza Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WANANCHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUTOIOGOPA MAHAKAMA

Na.Issack Gerald Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoiogopa mahakama kwa kuwa ipo kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wananchi katika kupatikana na kwa haki zao. Wito huo umetolewa na hakimu mwandamizi wa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda Mh.David Daniel Mbembela kupitia kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa cha Mpanda Radio. Aidha amewashauri wananchi kujenga tabia ya kufika katika mahakama kwa ajili ya kujifunza namna kesi zinavyoendeshwa mahakamani. Wakati huo huo Mh.Mbembela amesema serikali imeleta baraza la ardhi la wilaya mkoani Katavi kwa ajili ya kusikiliza migogoro na kesi zinazohusu masuala ya ardhi ambapo awali wakazi wa Mkoa wa Katavi walikuwa wakipata huduma hiyo wilayani Sumbawanga Rukwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AMEMTEUA DKT SLAA KUWA BALOZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe amemteua Dkt.Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi. Kwa mjibu wa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya Rais,Dkt.Wilbrod Peter Slaa ataapishwa baada ya taratibu kukamilika. Habari zaidi ni P5TANZANI ALIMITED

STENDI MPYA YA MABASI MPANDA KUANZA KUTUMIKA MWANZONI MWA 2018

Image
Na.Issack Gerald Mstahiki Meya wa M anispaa ya Mpanda mkoani katavi Willium Mbogo amesema stendi kuu ya mabasi ya kisasa inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwanzoni wa mwaka 2018. Mh.Mbogo amesema hatua iliyobaki ni ujenzi wa vibanda na kukamilisha huduma ya maji na umeme. Aidha amesema stendi hiyo itakuwa na uwezo wa kuingiza mabasi 60 kwa wakati mmoja   ambapo ametoa wito kwa wamiliki wote wa mabasi kununua mabasi yanayoenda na hadhi ya stendi. Mkoa wa Katavi umefikisha miaka mitano toka kuanzishwa kwake huku ukipiga hatua kubwa ya kimaendeleo ukilinganisha na mikoa mingine michanga. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

ROBO YA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMETUMIA SHILINGI MIL.50 KWA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI

Image
Na.Issack Gerald Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,imefanikiwa kutoa mkopo shilingi milioni hamsini kwa vikundi vya wanawake na vijana katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018. Hayo yamebainishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bi.Halima Kitumba wakati akizungumzia  kuhusu namna Halmshauri inavyotekeleza agizo la serikali kutumia asilimia 10 ya mapato ya ndani kuwawezesha wanawake na vijana. Katika mgao wa fedha hizo jumla ya vikundi 8 vya wanawake ambavyo vimepata shilingi milioni 29,700,000 huku vikundi 6 vya vijana vikipata miluioni 20,300,000. Aidha amesema katika robo ya pili inayoanzia mwezi Oktoba mwaka huu,wanatarajia kutumia shilingi milioni 50 kwa vikundi 19 ambapo mpaka sasa wametoa zaidi ya shilingi milioni 11,786,000/= zilizoelekezwa katika viwanda vidogo vidogo SIDO kwa ajili ya kununua vifaa vya uchakataji na kutoa mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali kwa wanawake na vijana waliopo Iko...

MKOANI KATAVI DIWANI JELA MIAKA 3 KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA

Image
Na. Issack Gerald Mahakama ya wilaya ya Mlele imemkumu kwenda jela diwani wa kata ya Katumba Senator  Jeriti Baraka kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa. Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Timothy Swai, mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Bahati Haule amedai mtuhumiwa alitenda kosa hilo 12.05.2016 kwa kuomba rushwa ya shilingi 500,000/=ili asimuhamishe mfugaji mmoja kwenye eneo lililozuiliwa na mahakama kuendesha shughuli za ufugaji. Taarifa iliyotolewa na  taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani katavi imesema mtuhumiwa amehukumiwa kwa makosa mawili tofauti ambapo kosa la kwanza ni kuomba rushwa na kosa la pili ni kupokea rushwa. Taarifa hiyo inaeleza kuwa kosa la kuomba rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kutoa faini ya shilingi 500,000/= au kifungo cha miaka mitatu na kosa la kupokea rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela bila faini. Katika taaifa ya Takukuru inaeleza kuwa b...

WAKAZI MKOANI KATAVI WAMESHAULIWA KUJIUNGA NA ASASI MBALIMBALI

Wananchi mkoani Katavi wameshauriwa kujiunga na asasi mbalimbali za kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi. Wito huo umetolewa na Emiliana Stanslaus, mkufunzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Girl Guides Association wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya You Report kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi. Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Katavi  Bi Anna Shumbi amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ili waweze kuandaa maisha yao ya baadae kulingana na dhima ya chama ya kuwainua kiuchumi Tanzania Girl Guides Association imelenga kuwaendeleza wasichana na wanawake  katika masuala  mbalimbali ya kijamii na kiuchumi Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RC KATAVI AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA KILIMO CHA PAMBA NA KOROSHO

Image
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amewataka wananchi kuchangamkia kulima kilimo cha korosho na pamba. Korosho  Ametoa kauli hiyo wakati wa kukabidhi hundi kwa vikundi vya akina mama na vijana wasiriamali  ambapo jumla ya milioni 37 zimetolewa kwa vikundi 12. Pamba Ameongeza kuwa  upatikanaji wa mbegu za mazao hayo ni wa uhakika na tayari mkoa wa Katavi umepokea tani 51 za mbegu ya pamba kutoka bodi ya pamba Tanzania Huu ni mkakati wa Mkoa wa katavi kuondoa utegemezi wa zao la tumbaku ambalo limekumbwa  na changamoto ya kukosekana wanunuzi . Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AWAONYA MASHA NA MSANDO,SOFIA SIMBA NAYE ASAMEHEWA WOTE WARUHUSIWA KUGOMBEA NYADHIFA MBALIMBALI NDANI YA CHAMA

Image
Na.Issack Gerald Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais John Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho leo kwenye mkutano mkuu wa NEC ambao umefanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Kutoka Kulia ni Bw.Laurenance Masha na anayefuata ni Alberto Msando Wanachama hao ambao wamehamia na kutangazwa leo ni Mwanasheria Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo,Mbunge wa zamani wa Nyamagana Laurent Masha aliyekuwa mwanachama wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi. Wengine ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye naye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa muda. Rais Magufuli amemaliza kwa kuwapa ruhusa ya kugombea nyadhifa mbalimbali ndani ya chama na kwenye maeneo yao. Kwa upande wake aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA Lawrence Masha ambaye ametangaza kukihama chama hiko hivi ka...

HABARI ZA HIVI PUNDE KUTOKA IKULU

Image
Serikali imekanusha taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurian Ndumbaro. Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ikulu ya rais Bw.Gerson Msigwa amesema taaifa hizo  sio za kweli  na  zipuuzwe . Taarifa hiyo inaeataka wananchi kuendelea kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya Serikali. Wakati huo huo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekumbushwa kumbushwa kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria. Hata hivyo,Serikali imesema itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED