WANANCHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUTOIOGOPA MAHAKAMA
Na.Issack Gerald
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa
kutoiogopa mahakama kwa kuwa ipo kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya
wananchi katika kupatikana na kwa haki zao.
Wito huo umetolewa na hakimu
mwandamizi wa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda Mh.David Daniel Mbembela kupitia
kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa cha Mpanda Radio.
Aidha amewashauri wananchi kujenga
tabia ya kufika katika mahakama kwa ajili ya kujifunza namna kesi
zinavyoendeshwa mahakamani.
Wakati huo huo Mh.Mbembela amesema
serikali imeleta baraza la ardhi la wilaya mkoani Katavi kwa ajili ya
kusikiliza migogoro na kesi zinazohusu masuala ya ardhi ambapo awali wakazi wa
Mkoa wa Katavi walikuwa wakipata huduma hiyo wilayani Sumbawanga Rukwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments