RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John
Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria
sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Mh.Uhuru Kenyatta.
Taarifa ya serikali ambayo imetolewa na Mkurugenzi,
Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi
imethibitisha hilo.
Mhe.Kenyatta
anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo jijini Nairobi ikiwa ni
baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini
humo.
Rais Uhuru Kenyatta atakuwa anaongoza Jamhuri ya
Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments