RAIS MAGUFULI ASISITIZA JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA
Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
amesisitiza kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe kwa sababu yeye
ndiye rais kwa sasa tofauti na zamani alipokuwa waziri.
Rais
amesema hayo mapema leo wakati akihutubia wananchi ambao wamejitokeza katika
ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) kampasi ya Mloganzila.
Aidha
rais Magufuli amesema Jengo hilo lazima libomolewe hata nusu ya jengo iliyopoo
katika hifadhi ya barabara huku akisema na kama ni kuondoa jengo lote basi inamaanisha
kuwa pia jengo la wizara ya maji nalo itabidhi liondolewe kwa kuwa sheria ni
msumeno.
Wakati
huo huo rais amesema wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa
fidia kwa sababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara na waliotakiwa kulipiwa
fidia walikwishalipwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments