RAIS MAGUFULI AWAONYA MASHA NA MSANDO,SOFIA SIMBA NAYE ASAMEHEWA WOTE WARUHUSIWA KUGOMBEA NYADHIFA MBALIMBALI NDANI YA CHAMA

Na.Issack Gerald
Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais John Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho leo kwenye mkutano mkuu wa NEC ambao umefanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Kutoka Kulia ni Bw.Laurenance Masha na anayefuata ni Alberto Msando
Wanachama hao ambao wamehamia na kutangazwa leo ni Mwanasheria Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo,Mbunge wa zamani wa Nyamagana Laurent Masha aliyekuwa mwanachama wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi.
Wengine ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye naye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa muda.
Rais Magufuli amemaliza kwa kuwapa ruhusa ya kugombea nyadhifa mbalimbali ndani ya chama na kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA Lawrence Masha ambaye ametangaza kukihama chama hiko hivi karibuni,ameomba kurejea CCM na kutumiwa pale atakapohitajika.
Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu cha leo Masha amesema yeye ni kada wa CCM kwani amezaliwa na kukulia ndani ya CCM,hivyo anaomba uongozi wa CCM umkubalie arudi nyumbani na kuitumikia CCM.
Hivi karibuni Lawrence Masha alitangaza kukihama chama cha CHADEMA akisema chama hicho hakina nia madhubuti ya kushika dola kama malengo ya vyama vya upinzani vingi duniani.
Wakati huo huo naye Mwanasheria maarufu nchini Alberto Msando ambaye amewahi kuwa mwanachama wa Chadema pamoja na ACT-Wazalendo ametangaza uamzi wa kuhamia ndani ya CCM katika mkutano wa leo.
Akizungumza katika mktano huo,Msando pia ameeleza kuwa alikuwa anaona anachelewa kujiunga na vijana wenzake kama Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde ambao mara zote amekuwa akiwaona wapo mstari wa mbele katika kupigania maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.
Aidha Msando ambaye amewahi kuwa mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema hii ni mara yake ya kwanza kuingia CCM kwa kuwa kwa sasa si aibu tena kwa mtu kujitambulisha kuwa ni mwana CCM kwani imesafishika kuliko ilivyokuwa awali ambapo ulikuwa ukionekana na nguo za CCM unazomewa mitaani.
 Katika hatua nyingine aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa chama cha CCM,Bi, Sophia Simba,kwa mara ya kwanza amezungumza baada ya CCM kumrudisha ndani ya chama.
Akizungumza na mwandishi wa habari,Sophia Simba amesema ni mapema mno kwa yeye kuzungumza zaidi lakini kikubwa anashukuru kwa chama kumrudisha baada ya kuomba radhi.
Sophia Simba alivuliwa uanachama wa CCM kutokana na utovu wa nidhamu,lakini leo chama kimeamua kumsamehe na kumrudisha baada ya kuandika barua kadhaa za kuomba radhi,zilizosomwa hadharani na Rais Magufuli.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA