HABARI ZA HIVI PUNDE KUTOKA IKULU
Serikali imekanusha taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya
kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe
Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurian Ndumbaro.
Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na mkurugenzi wa mawasiliano
ikulu ya rais Bw.Gerson Msigwa amesema taaifa hizo sio za kweli na zipuuzwe.
Taarifa hiyo inaeataka
wananchi kuendelea kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi
vya Serikali.
Wakati huo huo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekumbushwa kumbushwa
kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria.
Hata hivyo,Serikali
imesema itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu
wa sheria.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments