WANAHARAKATI WAMETAKA SHERIA ZINAZOHUSU WATU WENYE ULEMAVU ZIWE HAI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wanaharakati wa kutetea haki za watu
wenye ulemavu wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kusimamia kanuni
na sheria za nchi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu kama zilivyoainishwa
katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Wanaharakati hao wakiwemo mtandao wa
wazazi,Shivyawata, wajumbe wa baraza la watoto wilayani Mpanda na kamati ya
kulea baraza la watoto wenye ulemavu,wametoa kauli hiyo leo katika kikao cha
kujadili haki za watoto wenye ulemavu kikao ambacho kimefanyika mjini Mpanda.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa
Elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael
Fortunatus Jumbe pamoja na mambo mengine amesema semina ya leo inalenga
kufikisha elimu kwa wanaharakati ili washiriki kupaza sauti katika kutetea haki
za watu wenye ulemavu pamoja na kuwafichua watoto waluiofichwa majumbani.
Kwa mjibu wa vifungu vya sheria ya
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawaziri katika wizara husika
wanatakiwa kusimamia misingi yote inayompa haki za msingi mtu mwenye ulemavu
anapohitaji kuhudumiwa bila ubaguzi.
Naye mwenyekiti wa shirikisho la
vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi SHIVYAWATA Bw.Issack Lucas Mlela
ambaye pia ni mjumbe wa katamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu pamoja
na mambo mengine amesema sheria namba 9 ya mwaka 2010 inasimamia haki za watu
wenye ulemavu huku akisema wakati mwingine unyanyapaa nao unaanzia kwa ndugu
wenyewe kumnyanyapaa mwenye ulemavu suala ambalo halikubaliki na halifai kuigwa
na jamii.
Baadhi ya ibara zilizopo katika
katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ambazo zinazotakiwa zisimamiwe
vizuri ili watu wenye ulemavu wapate haki zao ni pamoja na ibara ya
4,20,26,27,28,31,32 na 34 ambavyo vinaitaka serikali ya Tanzania kutekeleza
haki zote za msingi kwa watu wenye ulemavu katika Nyanja mbalimbali ikiwemo
sekta ya afya,elimu,ajira na haki nyingine za kibinadamu.
Licha ya ibara hizo pia Tanzania ni
miongoni mwa nchi za jumuiya ya madola ambazo zilisaini mikataba mbalimbali kwa
ajili ya kusimamia na kutekeleza haki za watu wenye ulemavu.
Katika kipindi cha mwaka 2014 mpaka
2016 jumla ya watu wenye ulemavu 83 wakiwemo watoto wenye umri wa kwenda shule
wametetewa na mradi wa elimu jumuishi wilayani Mpanda na kupatiwa haki zao
muhimu kama elimu.
Harakati za kutetea,kuibua na
kuwezesha haki za watu wenye ulemavu hasa watoto Mkoani Katavi limekuwa
likiendshwa na shirika la kimataifa la IFI linaloundwa na washirika 3 ambao ni Free
Pentecostal Church Of Tanzania(FPCT),International centre on Disabilities(ICD)
na International Aid Services(IAS) ambapo kwa hapa nchini mradi wa elimu
Jumuishi upo katika mikoa ya Rukwa na Katavi pekee kati ya mikoa yote ya
Tanzania bara.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments