RAIS KENYATTA AMEANZA SAFARI YA PILI MUHULA WA PILI WA URAIS
Na.Issack Gerald
Hatimaye jana Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kwa muhula wa
pili wa miaka mitano katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Kasarani mwezi
mmoja baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi uliosusiwa na mpinzani mkuu Raila
Odinga.
Kulikuwa na nderemo na shangwe katika uwanja huo kutoka kwa
maelfu ya wananchi wengi wao wafuasi wa muungano wa chama tawala cha Jubilee
waliojaa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani.
Uwanja huo unaingiza watu 60,000 lakini habari zinasema
walioingia walikuwa 100,000.
Wageni waalikwa na watu mashuhuri wapatao 40 walihudhuria
sherehe hizo wakiwemo zaidi ya viongozi wakuu wa nchi 10.
Kenyatta,55,alishinda uchaguzi mkuu wa marudio wa Oktoba 26 kwa
asilimia 98.Uchaguzi huo ulifanyika baada ya matokeo ya ushindi wa Agosti 8
kufutwa na Mahakama ya Juu kwa maombi ya Odinga aliyewasilisha ushahidi wa
dosari na ukiukwaji wa katiba.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu ni
miongoni viongozi wa kimataifa waliohudhuria kiapo cha rais Kenyatta.
Habari zaidi na P5TANZANIA LIMITED
Comments