Posts

Showing posts from September, 2015

BUASARA,HEKIMA,LUGHA ZENYE HESHIMA ZATAKIWA KUTUMIKA MIKUTANO YA KAMPENI ZA KISIASA KATAVI

 Na.Issack Gerald-Katavi Busara,hekima na lugha zenye heshima   zimetakiwa kutumiwa na wanasiasa na jamii kwa ujumla katika kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi ili kuepuka kuitumbukiza nchi katika machafuko yanayohatarisha usalama wa Watanzania.

WAKAZI KATAVI WATAKA ELIMU NA KILIMO KUPEWA KIPAUMBELE NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Issack Gerald-MPANDA. ZIKIWA zimebakia siku 29 kufanyika kwa uchuguzi mkuu wa udiwani ubunge na raisi wananchi wameitaka   serikali ya awamu ya tano iboreshe   sekta ya elimu na kilimo.

AKAMATWA KITUO CHA POLISI AKISHUKIWA KUWA NA VIUNGO VYA BINADAMU

Na.Mwandishi -SINGIDA Jeshi lapolisi Mkoani Singida linamshikilia mtu mmoja anayefahamika wa jian la Magida Bundala   (30) Mkazi wa Mkoani humo wa kwa tuhuma za kukutwa   na mafuvu na viungo vinavyosadikiwa kuwa vya binadamu pamoja na nyara za serikali kinyume na sheria.

SIKUKUU YA EID KATAVI IBADA KUFANYIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI AZIMIO

Image
  Maandalizi yaibada ya hija Na.Issack Gerald-MPANDA WAUMINI wa dini ya kiislamu duniani kote leo wanasherehekea sikukuu ya Idd El Hajj baada ya kukamilika kwa ibada ya Hija.

RPC KATAVI KUHITISHA KIKAO CHA KUJADILI AMANI KESHO KIKISHIRIKISHA WAZEE MAARUFU

Na.Issack Gerald-KATAVI JESHI la polisi Mkoani Katavi kesho linatarajia kuwa na kikao maalumu cha kujadili mikakati ya kuimarisha amani na usalama wa nchi.

MWANAMKE AKAMATWA NSIMBO AKIANDIKA MAJINA NA NAMBA ZA VIPARATA

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la SALOME MAKALA, miaka 56, mkulima, mnyamwezi mkazi wa Mwenge Kitongoji cha Legezamwendo septemba 21 siku ya Jumatatu majira ya saa 4:00 kamili usiku alikamatwa akiwa anaorodhesha majina ya wanakijiji wa kijiji cha Mwenge Kata ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi kwenye daftari kwa kuandika majina yao na namba za vipalata vyao (kadi ya mpigakura).

UKATA WA PESA TANAPA KATAVI CHANZO CHA KUSHINDWA KUANDAA MAADHIMISHO SIKU YA TEMBO KIMKOA

NA.Issack Gerald-Katavi Uongozi wa hifadhi ya taifa ya wanyama ya Katavi umeshindwa kuandaa maadhimisho ya siku ya tembo kutokana na ukata wa kifedha ulipo katika shirika hilo mkoani hapa.

TWAWEZA WATANGAZA MATOTKEO YA UTAFITI CCM YAONGOZA,WAKAZI KATAVI WAONYA

Image
  Baadhi ya wakazi katika Picha wakijadili matokeo yaliyotangazwa na Taasisi ya twaweza jana Jijini Dar es Salaam Issack Gerald-Katavi Baadhi ya wakazi Mkoani Katavi wameitaka tume ya uchaguzi na tume ya haki za binadamu kufanya uchunguzi na kutorusu utafiti wa kutangaza matokeo kabla ya uchaguzi kufanyika.

UHABA WA MAJI ZAIDI YA WAKAZI 750 WAATHIRIKA

Issack Gerald-Katavi ZAIDI YA WAKAZI 750 waishio mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo wanakabiliwa na   ukosefu wa   maji safi na salama hali inayosababisha kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

ZAIDI YA SILAHA 17 ZAKAMATWA,WATUHUMIWA WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Issack Gerald-Katavi Zaidi ya silaha 17 zimekamatwa na kusalimishwa kwa jeshi la polisi Mkoani Katavi huku watu wanne wakifikishwa Mahakamani kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Septemba Mwaka huu.

KATAVI KUFANYA MKUTANO WA MAZINGIRA WIKI IJAYO

Issack Gerald-MPANDA . MKOA Wa Katavi unatarajia kufanya Mkutano na wadau wa mazingira   ili kutafuta suluhisho la kukabiliana na uhalibifu wa   Mazingira uliokithiri Katika   maeneo mbalimbali Mkoani hapa.

MWANAUME MMOJA AKUTWA AKIWA AMEKUFA WILAYANI MLELE

Issack Gerald-KATAVI MTU Mmoja jinsia ya Kiume ambae hakutambulika jina wala umri wake ameuwawa   kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika kijiji cha tumaini kata ya Itenka Wilayani Mlele.

WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA SIKU YA DEMOKRASIA DUNIANI KATIKA MAMBO YENYE TIJA KWA WATANZANIA

NA.Issack Gerald-MPANDA Watanzania wameshauliwa kutumia maadhimisho ya siku ya demokrasia duniani kufanya mambo yenye tija   kwa umma wa watanzania.

PICHA ZA MACHINJIO YA MPANDA HOTEL YALIYOKUWA YAMEZUIWA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI

Image
Moja ya bucha manispaa ya Mpanda Watu wakijipatia kitoweo baada  ya machnjio kufunguliwa jana Benezeti Kusaya mwenyekiti wa wafanyakazi machinjioni Jengo la machinjio Mpanda Nembo ya mamlaka ya chakula na dawa Tanzania TFDA iliyokuwa imebandikwa katika kuta za machinjio baada ya machinjio hayo kufungwa Mazingira ya machinjio Sehemu wanakopanga nyama asubuhi Vijana baada ya kikao cha kuhamasisha usafi machinjioni Shimo la kutunza uchafu machinjioni lililokuwa limejaa na kuanza kutiririsha uchafu mtoni

SERIKALI YASHAULIWA KUWEKA ULINZI VITUO VYA AFYA

NA.Issack Gerald-MPANDA. SERIKALI imeshauriwa kuweka ulinzi wa uhakika katika vituo vya afya    hasa katika   maeneo ya vijijini sambamba na kujenga nyumba za watumishi wanaotoa huduma katika Vituo hivyo.

CWT KATAVI KUDAI ZAIDI YA MIL..379

Na.Issack Gerald-KATAVI HALMASHAURI Za Wilaya ya Mpanda,Nsimbo na Manispaa ya Mpanda zimetakiwa kulipa madeni yanayodaiwa na walimu wa shule za Msingi na Sekondari Mkoani hapa.

MACHINJIO YA WANYAMA MPANDA YAFUNGULIWA

Image
  Moja ya bucha Manispaa ya Mpanda Rikiuza nyama baada ya machinjio kufunguliwa jana Nembo ya Mamlaka ya chakula na dawa iliyokuwa imewekwa baadaya kufungwa kwa machinjio wiki iliyopita Watu wakipata kitoweo machinjioni leo Mwenyekiti wa wafanyakazi wa machinjio ya Mpanda Hoteli Bw.Benezeti Kusaya akizungmza katika kikao ambacho kimefanyika leo na vijana wanaotegemea ajira ya machinjio akihamasisha zaidi kufanyika usafi mara kwa mara NA.Issack Gerald- MPANDA Machinjio ya wanyama yaliyopo kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda yaliyokuwa yamefungwa na Mamlaka ya chakula na dawa Tanzania TFDA kutokana na uwepo wa   uchafu na miundombinu mibovu katika machinjio hayo yamefunguliwa.

WANAFUNZI WATAKA AHADI YA ELIMU BURE ITEKELEZWE

Na.Issack Gerald-Mpanda BAADHI ya wanafunzi wa darasa la saba wanaohitimu elimu ya msingi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamewataka wagombea wa nafasi mbalimbali  za uongozi watakaoshinda katika uchaguzi wa mwezi Oktoba kuhakikisha wanatekeleza ahadi ya kutoa elimu bure. Kauli hiyo imetolewa leo na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi zilizopo katika Manispaa ya Mpanda ikiwemo shule ya Msingi Kashato. Wakati huo huo Msimamizi mkuu wa mitihani katika shule ya Msingi Kashato mwalimu Sekela Mayeji, amesema Jumla ya wanafunzi 108 wamefanya mtihani katika hali ya  utulivu. Katika mtihani huo Jumla ya wanafunzi wapatao laki saba kote nchini wanatarajia kumaliza mitihani ya kuhitimu darasa la saba leo.