UHABA WA MAJI ZAIDI YA WAKAZI 750 WAATHIRIKA
Issack Gerald-Katavi
ZAIDI YA WAKAZI 750 waishio mtaa wa Kampuni kata ya
Misunkumilo wanakabiliwa na ukosefu
wa maji safi na salama hali
inayosababisha kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya shughuli
nyingine za maendeleo.
Mapema leo wakazi hao wakiongea na mpanda fm wamesema
kero ya ukosefu wa maji ni ya muda mrefu ambapo mpaka sasa wana kisima kimoja
ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya wananchi katika eneo hilo.
Aidha baadhi yao wamewatuhumu
viongozi na wanasiasa kutumia kero ya maji kama chambo cha kujipatia kura na
kusahau ahadi hizo mala tu wanapo shika madaraka.
Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa huo Bw James Solomoni
amewataka wananchi wa eneo hilo kuwa na subira wakati serikali ikikabiliana na
utatuzi wa changamoto hizo.
Comments