ZAIDI YA SILAHA 17 ZAKAMATWA,WATUHUMIWA WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI
Issack
Gerald-Katavi
Zaidi ya
silaha 17 zimekamatwa na kusalimishwa kwa jeshi la polisi Mkoani Katavi huku watu
wanne wakifikishwa Mahakamani kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Septemba Mwaka
huu.
Hayo
yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhairi Kidavashari wakati
akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mafanikio ya agizo la kusalimisha silaha
alilolitangza mwezi Juni mwaka huu akiwataka wanaomiliki silaha kinyume na
sheria kuzisalimisha.
Katika
hatua nyingine akizungumzia siku ya amani duniani amesema kufuatwa kwa sheria
na ushirikiano kati ya Jeshi la polisi na raia kutachangia amani kudumu Mkoani
Katavi na Tanzania kwa ujumla.
Wakati huo huo akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es
salaam Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali
imejipanga kuhakikisha inalinda Amani na kuheshimu demokrasia hasusani katika
kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu.
Siku ya
amani duniani inayoadhimishwa kimataifa
kila ifikapo Septemba 21 ya kila mwaka, kitaifa
imeadhimishwa Mkoani Mwanza wakiti kimataifa maadhimisho yakifanyika
Nchini Rwanda.
Kauli mbiu
katika maadhimisho ya siku ya amani mwaka huu ni ‘’Ushirikiano wa amani, utu kwa wote”
Comments