BUASARA,HEKIMA,LUGHA ZENYE HESHIMA ZATAKIWA KUTUMIKA MIKUTANO YA KAMPENI ZA KISIASA KATAVI
Na.Issack Gerald-Katavi
Busara,hekima na lugha zenye heshima zimetakiwa kutumiwa na wanasiasa na jamii kwa
ujumla katika kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi ili kuepuka kuitumbukiza
nchi katika machafuko yanayohatarisha usalama wa Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kamanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari katika kikao maalumu na
wanasiasa,viongozi wa dini na wazee maarufu ambacho kimefanyika katika makao
makuu ya Polisi Mkoani Katavi.
Kwa upande wa washiriki wa kikao
hicho wamesema kuwa viashiria vya uvunjifu wa amani Mkoani Katavi katika
kipindi cha Kampeni vimeshamiri ambapo wameliomba jeshi la polisi kuthibiti
hali hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya siasa.
Wakati huohuo vyama vinavyoonywa
kufanya vurugu kutokana na kurushiana maneno ya kejeli ni pamoja na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema na Chama cha Mapinduzi CCM.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa
vyama vya saiasa wamelitaka jeshi la polisi kutenda haki kwa kila chama katika
kushugulikia malalamiko yanayowasilishwa kwao na kukomesha misemo inayotumiwa
na Chama cha Mapinduzi CCM kuwa wao ndiyo chama chenye dola na hakuna wa
kuwatisha kauli ambayo inaonekana kuwakwaza baadhi ya wafuasi wa vyama vingine.
Kaikao hicho ni mwendelezo wa kikao
kama hicho kilichofanyika Septemba 11 mwaka huu ambapo pia kikao kingine
kinatarajiwa kufanyika Oktoba 9 wiki mbili kabla ya uchaguzi.
Comments