WAKAZI KATAVI WATAKA ELIMU NA KILIMO KUPEWA KIPAUMBELE NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO
Issack Gerald-MPANDA.
ZIKIWA
zimebakia siku 29 kufanyika kwa uchuguzi mkuu wa udiwani ubunge na raisi
wananchi wameitaka serikali ya awamu ya
tano iboreshe sekta ya elimu na kilimo.
Hayo
yamesemwa leo na wakazi wa maeneo mbalimbali katika katika mahojiano na P5 TANZANIA ambapo imebainika kuwa
changamoto hizo ni kikwazo kwa maendeleo ya taifa.
Wameongeza
kuwa serikali ijayo ihakikishe inafungua masoko ya ndani na mpenyo wa masoko ya
nje ili mkulima kuepuka unyonyaji unao
fanywa na wafanyabiashara wakubwa kwa kujipangia bei kwa kisingizio cha uhaba
wa masoko.
Hata
hivyo wameipongeza serikali ya awamu ya
nne kwa kuboresha miundo mbinu ya shule ikiwemo ujenzi wa maabara huku
wakiongeza kuwa ili elimu iwe na tija serikali ya awamu ya tano itatue vikwazo
vya upatikanaji wa ajira.
Comments