UKATA WA PESA TANAPA KATAVI CHANZO CHA KUSHINDWA KUANDAA MAADHIMISHO SIKU YA TEMBO KIMKOA
NA.Issack Gerald-Katavi
Uongozi wa hifadhi ya taifa ya wanyama
ya Katavi umeshindwa kuandaa maadhimisho ya siku ya tembo kutokana na ukata wa
kifedha ulipo katika shirika hilo mkoani hapa.
Hayo yamebainishwa leo na mhifadhi
Mkuu idara ya ujirani mwema katika hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Katavi Bw.David
Kadomo wakati akizungumza na P5 TANZANIA
kuhusu siku ya tembo kitaifa ambayo imeadhimishwa leo.
Aidha amesema elimu inaendelea
kutolewa kwa jamii kupambana na kutokomeza ujangili dhidi ya tembo na wanyama wengine.
Maliasili
na Utalii ikishirikiana na Shirika la Uhifadhi Duniani WWF ofisi ya Tanzania
kwa pamoja wanaadhimisha siku ya tembo kitaifa mwaka huu kwa kujadili na
wadau mbali mbali kuhusu kuwaokoa wanyama Tembo kupitia vyombo vya habari hapa
nchini.
Maadhimisho
haya yanatokana na mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa
kuzuia biashara ya Wanyamapori na viumbe walioko hatarini kutoweka uliofanyika
mwaka 2010 katika mji wa Doha nchini Quatar.
Nchi
37 zilizojaliwa kuwa na tembo barani Afrika zilikutana, na kupitisha mpango
mkakati wa kuhifadhi tembo barani Afrika Ambapo Mwaka uliofuatia wa 2011 Tanzania
ilianza kutekeleza mpango mkakati maalum wa uhifadhi wa Tembo.
Tanzania
inasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa wa wanyamapori barani Afrika na
Ulimwenguni kote,ikiwa ni nchi ya pili
duniani kwa kuwa na rasilimali nyingi asili.
Katika
kuhakikisha kuwa wanyamapori hususani Tembo wanalindwa, Tanzania imetenga zaidi
ya asilimia 24 ya ardhi yake kwa ajili ya uhifadhi.
Kipaumbele
cha Mpango Mkakati wa uhifadhi ni pamoja na; kulinda shoroba za wanyamapori
hususani Tembo; kupunguza migogoro kati ya wananchi na Tembo; kufanya tafiti za
uhifadhi wa tembo na kushirikisha wadau mbalimbali katika kuhifadhi Tembo.
Serikali
imekua ikifanya shughuli za uhifadhi wa wanyamapori kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali, mashirika ya kimataifa kama WWF,
taasisi zisizo za kiserikali, wafanyabiashara, taasisi za kidini na wananchi
kwa ujumla.
Comments