TWAWEZA WATANGAZA MATOTKEO YA UTAFITI CCM YAONGOZA,WAKAZI KATAVI WAONYA
Baadhi ya wakazi katika Picha wakijadili matokeo yaliyotangazwa na Taasisi ya twaweza jana Jijini Dar es Salaam |
Issack Gerald-Katavi
Baadhi ya wakazi Mkoani Katavi wameitaka tume ya uchaguzi na
tume ya haki za binadamu kufanya uchunguzi na kutorusu utafiti wa kutangaza
matokeo kabla ya uchaguzi kufanyika.
Wakizungumza na P5 TANZANIA wakazi hao wamesema kutoa matokeo
ya utafiti kabla ya uchaguzi kunaweza kuligawa taifa na kupelekea uvunjifu wa
amani nchini.
Kauli ya wakazi hao inakuja ikiwa ni saa chache baada ya
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza kutangaza matokeo ya utafiti wake.
Utafiti huo umeonesha kuwa endapo uchaguzi ungefanyika mwezi mmoja
uliopita, mgombea urais wa CCM John Magufuli angepata ushindi kwa asilimia 65.
Matokeo ya utafiti huo ambao
umetolewa leo jijini Dar es salaam unaonesha pia kuwa wagombea wa CCM
katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na ubunge na udiwani CCM inaongoza.
Katika ngazi ya udiwani CCM imeongoza kwa asilimia 60 ikifuatiwa
na CHADEMA asilimia 24 na ngazi ya ubunge CCM imeongoza kwa asilimia 60
ikifuatiwa na CHADEMA yenye asilimia 26, wakatika katika ngazi ya urais bila
kujali mgombea, CCM imeongoza kwa asilimia 66 ikifuatiwa na CHADEMA asilimia 22
huku chama cha ACT Wazalendo kikifuatia kwa kuungwa mkono na wananchi kwa zaidi
ya asilimia 1%.
Siku chache zilizopita Asasi za kiraia AZAKI ikiwemo
TWAWEZA, zilizindua ilani ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 na kuzuia kauli zenye mwelekeo wa uchochezi na utabiri wa matokeo
ya uchaguzi wa mwaka huu.
Comments