MWANAMKE AKAMATWA NSIMBO AKIANDIKA MAJINA NA NAMBA ZA VIPARATA
Mtu mmoja aliyejulikana kwa
jina la SALOME MAKALA, miaka 56, mkulima, mnyamwezi mkazi wa Mwenge Kitongoji cha
Legezamwendo septemba 21 siku ya Jumatatu majira ya saa 4:00 kamili usiku alikamatwa
akiwa anaorodhesha majina ya wanakijiji wa kijiji cha Mwenge Kata ya Nsimbo
Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi kwenye daftari kwa kuandika majina yao na namba
za vipalata vyao (kadi ya mpigakura).
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari
alisema kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa toka kwa mgombea ubunge wa Jimbo
la Nsimbo kwa tiketi ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) GERALD KITABU kuwa kuna mkazi mmoja aliyefahamika
kwa jina la SALOME MAKALA ameonekana akiorodhesha majina ya wananchi wa eneo la
Kijiji cha Mwenge pamoja na namba zao za vipalata.
Kufuatia
taarifa hiyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema walifanikiwia kufika
eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa huyo kisha kumfikisha kituo cha Polisi
Nsimbo.
Katika
mahojiano ya awali, mtuhumiwa alieleza kuwa lilikuwa ni zoezi la kukusanya
taarifa za wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (CWT) wa eneo lao ili kuwa
na kumbukumbu.
Hata
hivyo, upelelezi wa shauri hili bado unaendelea.
Comments