KATAVI KUFANYA MKUTANO WA MAZINGIRA WIKI IJAYO


Issack Gerald-MPANDA.
MKOA Wa Katavi unatarajia kufanya Mkutano na wadau wa mazingira  ili kutafuta suluhisho la kukabiliana na uhalibifu wa  Mazingira uliokithiri Katika  maeneo mbalimbali Mkoani hapa.

Kwa Mjibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kaimu Katibu tawala Mkoa wa Katavi  Bwana Salum Shilingi, Mkutano huo utafanyika sept 25 Mwaka huu Katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Maji Mjini Mpanda.
Mkoa wa Katavi ni Miongoni mwa Mikoa ya hapa nchini inayokabiliwa na ongezeko kubwa la uhalibifu wa Mazingira ikiwemo wafugaji kuvamia vyanzo vya maji na hifadhi za taifa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA