MWANAUME MMOJA AKUTWA AKIWA AMEKUFA WILAYANI MLELE
Issack Gerald-KATAVI
MTU Mmoja jinsia ya Kiume ambae
hakutambulika jina wala umri wake ameuwawa
kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika kijiji cha tumaini kata ya
Itenka Wilayani Mlele.
Taarifa ya Jeshi la polisi kwa vyombo
vya habari imesema tukio hilo limetokea Usiku wa kuamkia juzi ambapo mwili wa
marehemu ulichomwa moto na watu wasiojulikana baada ya kutekeleza Mauaji hayo.
Katika tukio linguine mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Obed Yoram (35) Muha Mkazi wa Kijiji cha Vikonge Kata
ya Mpanda ndogo wilayani Mpanda ameuwawa kwa kupigwa na fimbo na kasha mwili
wake kuchomwa moto.
Kufuatia Matukio hayo Jeshi la polisi
Mkoani hapa linaendelea na Msako ili kuwabaini watuhumiwa wa Makosa mbalimbali
ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Comments