WANAFUNZI WATAKA AHADI YA ELIMU BURE ITEKELEZWE
Na.Issack Gerald-Mpanda
BAADHI ya wanafunzi
wa darasa la saba wanaohitimu elimu ya msingi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi
wamewataka wagombea wa nafasi mbalimbali
za uongozi watakaoshinda katika uchaguzi wa mwezi Oktoba kuhakikisha
wanatekeleza ahadi ya kutoa elimu bure.
Kauli hiyo imetolewa
leo na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi zilizopo katika Manispaa ya
Mpanda ikiwemo shule ya Msingi Kashato.
Wakati huo huo
Msimamizi mkuu wa mitihani katika shule ya Msingi Kashato mwalimu Sekela Mayeji,
amesema Jumla ya wanafunzi 108 wamefanya mtihani katika hali ya utulivu.
Katika mtihani
huo Jumla ya wanafunzi wapatao laki saba kote nchini wanatarajia kumaliza mitihani
ya kuhitimu darasa la saba leo.
Comments