CWT KATAVI KUDAI ZAIDI YA MIL..379
Na.Issack Gerald-KATAVI
HALMASHAURI Za Wilaya ya Mpanda,Nsimbo na Manispaa ya Mpanda
zimetakiwa kulipa madeni yanayodaiwa na walimu wa shule za Msingi na Sekondari
Mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha
walimu Tanzania CWT Mkoa Bwana John Gregory Mshota amesema halmashauri hizo
zinadaiwa na walimu zaidi ya shilingi Milioni 379 kutokana na malimbikizo ya
malipo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Bwana Mshota amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dr Ibrahimu Msengi Kuingilia Kati suala la Upotevu wa hati za Mshara wa walimu Waliokuwa halmashauri ya Mji Mpanda Kabla ya
kuwa manispaa kwa Mwezi Augost 2008
,Kama alivyoahidi Mwezi February mwaka huu, Katika kikao cha pamoja na walimu
wa shule za Msingi.
Comments