WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA SIKU YA DEMOKRASIA DUNIANI KATIKA MAMBO YENYE TIJA KWA WATANZANIA
NA.Issack Gerald-MPANDA
Watanzania wameshauliwa kutumia
maadhimisho ya siku ya demokrasia duniani kufanya mambo yenye tija kwa umma wa watanzania.
Hayo yamebainishwa leo na baadhi ya
wakazi katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wakati wa mahojiano na Mpanda
Radio.
Wamesema kuwa ni muda mwafaka kwa
watanzania kutafakari mafanikio na changamoto
za kidemkorasia hapa nchini ili watanzania waendelee kuwa wamoja na kudumisha
amani.
Kipindi pia kimezungumza na wazee wa
maeneo mbalimbali ambapo Mzee Ramadhani Salum Songolo na Issack Mlela ambao nao
wametoa maoni yao kuhusu siku ya demokrasia duniani.
Siku ya demokrasia duniani
huadhimishwa kila mwaka ifikapo Septemba 15.
Comments