SERIKALI YASHAULIWA KUWEKA ULINZI VITUO VYA AFYA
NA.Issack Gerald-MPANDA.
SERIKALI imeshauriwa kuweka ulinzi wa uhakika
katika vituo vya afya hasa katika maeneo ya vijijini sambamba na kujenga nyumba
za watumishi wanaotoa huduma katika Vituo hivyo.
Ushauri huo umetolewa na wauguzi katika zahanati ya sibwesa
ikiwa ni wiki tatu zimepita baada ya tukio la mwenyekiti wa serikali ya Kijiji
hicho kumpiga Mganga wa Kituo hicho kwa madai ya Kumtolea lugha chafu Mgonjwa
aliyefika katika zahati hiyo Kupata Matibu.
Kufuatia tukio hilo Uongozi wa hospitali ya Wilaya ya Mpanda
ulilazimika Kufunga kituo hicho ili kupisha uchunguzi wa chanzo cha Ugomvi huo
ambapo hata hivyo kituo hicho kimefunguliwa kuendelea na utoaji wa huduma.
Comments