MACHINJIO YA WANYAMA MPANDA YAFUNGULIWA
Moja ya bucha Manispaa ya Mpanda Rikiuza nyama baada ya machinjio kufunguliwa jana |
Nembo ya Mamlaka ya chakula na dawa iliyokuwa imewekwa baadaya kufungwa kwa machinjio wiki iliyopita |
Watu wakipata kitoweo machinjioni leo |
NA.Issack Gerald-MPANDA
Machinjio ya wanyama yaliyopo kata ya
Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda yaliyokuwa yamefungwa na Mamlaka ya chakula na
dawa Tanzania TFDA kutokana na uwepo wa uchafu na miundombinu mibovu katika machinjio
hayo yamefunguliwa.
Wakizungmza na Mpanda Radio Vijana na
wafanyabiashara wanaofanya shughuli
mbalimba katika Machinjio hayo wameishukuru TFDA kwa kufungua machinjio hayo.
Wakati huohuo mwenyekiti wa
wafanyakazi machinjioni Bw.Benezeti Kusaya amewasisitiza wafanyakazi wote kushirikiana
kwa pamoja kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi ili kuepuka kufungiwa tena
sambamba na kusababisha mlipuko wa ugonjwa kipindupindu.
Machinjio ya Mpanda Hoteli yalifungwa
wiki iliyopita na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kufuatia kuwepo mazingira
machafu na miundombinu mibovu
inayohatarisha afya ya mlaji.
Comments