SIKUKUU YA EID KATAVI IBADA KUFANYIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI AZIMIO
WAUMINI wa dini ya kiislamu duniani kote leo wanasherehekea
sikukuu ya Idd El Hajj baada ya kukamilika kwa ibada ya Hija.
Akizungumza
na P5 TANZANIA ,Kaimu shehe wa Mkoa
wa Katavi Shehe Said Omary amesema kuwa ibada ya Eid inatarajia kufanyika leo katika
viwanja vya Shule ya msingi Azimio vilivyopo Manispaa ya Mpanda.
Wakati huo huo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema
mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za Idd El Hajj leo ni Makamu wa Rais,
Dk Mohammed Gharib Bilal yanayofanyika kitaifa mkoani Mara.
Comments