RPC KATAVI KUHITISHA KIKAO CHA KUJADILI AMANI KESHO KIKISHIRIKISHA WAZEE MAARUFU
Na.Issack Gerald-KATAVI
JESHI
la polisi Mkoani Katavi kesho linatarajia kuwa na kikao maalumu cha kujadili
mikakati ya kuimarisha amani na usalama wa nchi.
Kikao
hicho ambacho kinaandaliwa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi kikishirikisha
wazee maarufu,wanasiasa na viongozi wa dini kinalenga kujadili namna ya
kuakikisha usalama unakuwepo kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba
mwaka huu.
Miongoni
mwa ambayo yamekuwa yakitajwa kuhatarisha amani ya nchi ni pamoja na Lugha za
uchochezi kutoka kwa wanasiasa na wafuasi wao na kutozingatia taratibu na
miongozo ya uendeshaji kampeni.
Kikao
hicho ni cha pili baada ya kile kilichofanyika Septemba 11 ambapo pia
wanatarajia kujadili ikiwa yale yaliyojadiliwa katika kikao kilichopita
yametekelezwa.
Comments