WAZIRI MKUU AAGIZA VYAMA VIWILI VICHUNGUZWE
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kassim Majaliwa amebaini Kasoro nyingi katika Vyama Vikuu vya Ushirika
vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike.
Majaliwa ametoa agizo hilo wakati
akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga katika viwanja vya CCM,mjini
Mbinga ambapo amesema timu ya uchunguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
itakiangalia chama hicho na kukifumua chote.
Kwa upande mwingine Waziri Mkuu
amewaamuru viongozi wote wa zamani na wa
sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya huku OCD akihakikisha ofisi za vyama hivyo
hazifunguliwi hadi kazi ya uchunguzi itakapoanza ili kuepuka kubadilisha
nyaraka katika ofisi zao.
Aidha Mh.Majaliwa amesema wote
watakaobainika kuhusika katika kasoro hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Waziri Mkuu pia ameeleza kuwa
Serikali imeamua kuboresha ufanisi katika mazao matano ya biashara ambayo ni
Pamba, Kahawa,Chai,Korosho na Tumbaku kwa sababu yanaliingizia Taifa fedha za
kigeni.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments