MATUKIO 18742 YALITIKISA MKOANI KATAVI KWA MWAKA 2017
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
limesema makosa 18742 ya kiuharifu yameripotiwa katika kipindi cha mwezi
Januari mpaka Desemba mwaka 2017.
Akitoa ripoti ya mwaka 2017 kuhusu
hali ya usalama,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema
utofauti wa matukio ya uhalifu kati ya mwaka 2017 na 2016 ni 1101 ambapo kwa
mwaka 2016 kulikuwa na matukio 17641 yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi.
Kamanda Nyanda amesema matukio
yaliyochukua nafasi kubwa yanahusu usalama barabarani mwaka 2017 yaliripotiwa
matukio 11592 sawa na asilimia 62 ya matukio yote huku ajali zikiwa 55 kwa
mwaka 2017 na 65 kwa mwaka 2016.
Aidha Kamanda Nyanda amesema matukio
ya Jinai yaliyoripotiwa Kwa kipindi cha Januari mpaka Desember 2017 ni 7150
ikilinganishwa na matukio 7549 yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2016 na
kuwa na upungufu wa matukio ya jinai 399 sawa na asilimia 5.3 ya matukio yote.
Amesema matukio makubwa 901 ya Jinai
yaliripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2017 ambapo mwaka 2016 kuliripotiwa matukio
973 na kuwa na upungufu wa matukio 72 sawa na asilimia 7.4 ya matukio yote
makubwa ya jinai.
Katika hatua nyingine taarifa ya
Kamanda Nyanda inaonesha Jumla ya silaha 09 zikiwemo SMG 02 na Gobore 07
zilisalimishwa kwa mwaka 2016 huku kwa mwaka 2017 jumla ya silaha 16 zikiwemo
SMG 05,Short gun 02 na Gobore 12 zikisalimishwa.
Katika hatua nyingine katika kipindi
cha mwaka 2017 jeshi la polisi limetembelea vijiji vyote 177 mkoani katavi huku
katika kipindi cha mwaka 2018 wakitarajia kutembelea vitongoji vyote 933 ili
kutoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi.
Hata hivyo kuanzia Januari 28 mpaka
30 mwaka huu,jeshi la polisi linatarajia kuendesha zoezi la uwekaji wa alama
maalumu ya utambulisho wa silaha za kiraia na kuwataka wamiliki wote wa silaha
za kiraia kufika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments