RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI NAIBU WAZIRI WA MADINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli leo amemteua Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.
Mhe.Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na alikuwa Mwenyekiti wa
kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.
Kufuatia uteuzi huo,Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na
Naibu Mawaziri wawili.
Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano
ya rais Ikulu Gerson Msigwa amesema, rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa
lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.
Mhe.Doto Mashaka Biteko anatarajiwa kuapishwa Jumatatu Januari 08
Januari mwaka huu Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments