ANAYEJIHUSISHA NA UUZAJI VIUNGO VYA BINADAMU ADAKWA NA POLISI NCHINI CYPRUS,KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Polisi nchini Cyprus wamesema
wanamshikilia raia mmoja wa Israel Moshe Harel anayetuhumiwa kufanya biashara
ya viungo vya binadam.
Harel amehusishwa kufanya biashara ya
figo kwa matariji wa Israel takriban miaka kumi sasa.
Amehusishwa kuchukua figo za raia wa
Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipa
chochote.
Msemaji wa polisi nchini Cyprus
amesema mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca mwezi Desemba mwaka jana
ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne ya wiki ijayo kujibu mashtaka
yanayomkabili.
Wakati huo hupo Harel anahitajika kwa
makosa kama hayo nchini Kosovo ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Chanzo:bbc
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments