MAMLUKI WADAIWA KUINGIZWA UGAWAJI WA VIWANJA KWA WAKAZI WA MSASANI NA TAMBUKARELI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Wakazi wengi wa Mtaa wa Msasani na
Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hawajahama kupisha mipaka ya
hifadhi ya reli licha ya kutakiwa kuondoka kabla ya mwezi Januari mwaka huu.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti
wamesema,baadhi yao wamesema hawajaondoka katika maeneo hayo kutokana na
ukosefu wa viwanja huku wakisema baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa huo
wamejigawia kiwanja zaidi ya kimoja kinyume na utaratibu ulivyopangwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa
Msasani Jonard Makoli amekanusha wajumbe wa serikali kujipatia viwanja zaidi ya
kimoja ambapo amesema mchakato wa majina ya wanaotakiwa kupata viwanja ilipitia
katika vikao na mikutano ya hadhara.
Wakati huo huo Makoli amesema
Manispaa ya Mpanda kuchelewa kupima viwanja kumesababisha zaidi ya wakazi 200
kukosa viwanja vya kujengea makazi yao mpaka sasa.
Hata hivyo Bw.Makoli amesema kamati
iliyokuwa inafuatilia rufaani inayopinga bomoabomoa haijajulikana ni lini
itatoa taarifa rasmi ya hatua iliyofikia katika kipindi cha mwaka 2018 ambapo
mara ya mwisho kamati ilitakiwa kukamilisha malipo ya ada ya rufaani mwezi
Novemba mwaka jana.
Zaidi ya wakazi 280 wa mitaa ya
Msasani na Tambukareli wameathiriwa na tangazo la bomoabomoa lililotolewa na
mwishoni mwa mwaka jana na mamlaka inayohusika na reli Tanzania.
Hata hivyo huenda Shirika la reli
Tanzania TRL likaanza kuendesha bomoabomoa kwa kuwa muda uliotolewa kwa wakazi
hao kuishi katika maeneo hayo ulikwisha Tangu mwezi Desemba mwaka jana.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments