CWT KATAVI CHAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUTENGA SHILINGI BIL.200 KULIPA MADENI YA WATUMISHI
Chama cha Walimu CWT mkoa wa Katavi
kimempongeza rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kutangaza kutoa fedha
Shilingi bilioni 200 ili zilipe madeni ya ndani yakiwemo ya walimu.
Kauli ya pongezi imetolewa na katibu
wa chama hicho mwalimu Hamis Chinahova ambapo amesema hatua ya serikali kulipa
madeni hayo italeta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.
Katika hatua nyingine amewataka
waalimu kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuleta tija kwa
jamii na taifa kwa ujumla.
Mwaka 2017 walimu nchini Tanzania
walitishia kugoma kwa kile walichokitaja kuwa ni kukithiri kwa madai dhidi ya
serikali wakisema inawavunja molali ya kufanya kazi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments