MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE APOKEA KWA MASIKITIKO KIFO CHA MKEWE
Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge
Ngombale Mwiru leo amepewa taarifa za kifo cha mke wake Pares Mwiru ambazo
imeelezwa kuwa amezipokea kwa mshtuko mkubwa.
Kingunge ambaye amelazwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela akipatiwa matibabu baada ya
kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Kijitonyama,alifanyiwa upasuaji Januari 4
mwaka huu.
Mtoto wa mwanasiasa huyo Kinje Mwiru
amesema wamempa taarifa baba yao saa tano asubuhi leo huku Kinje akisema kwa
sasa wamemuacha baba yake apumzike ili aweze kuwapatia mwongozo nini kifanyike
baada ya kifo cha mke wake.
Pares alifariki Januari 4 saa nane
mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa tangu alipofikishwa Muhimbili
Oktoba 3,mwaka jana.
Kwa mjibu wa Ofisa Uhusiano wa MNH
John Stephen amesema kwa sasa afya ya mwanasiasa huyo mkongwe imeimarika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments