WABUNGE WALIOJIUZULU VYAMA VYA UPINZANI NA KUJIUNGA CCM WAPITISHWA KUGOMBE KATIKA MAJIMBO YAO

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewarudisha waliokuwa wabunge wa upinzani kugombea majimbo ya Siha na Kinondoni baada ya wabunge hao kuijiunga na chama hicho.
Uthibitisho huo umeelezwa katika taarifa ambayo imetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Hamphrey Polepole imesema,baada ya tafakuri na tathimini ya kina.
Polepole amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dk Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro na Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.
NEC imesema wagombea wa ubunge wanaelekezwa kufika katika ofisi za CCM katika mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM wa mikoa hiyo Jumanne ijayo ya Januari 9 bila kukosa.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA