ZAIDI KAYA 40 ZINALALA NJE MKOANI KATAVI
Issack Gerald-Mpanda Katavi
Zaidi ya kaya 40 katika manispaa ya
Mpanda hazina mahali pa kuishi baada ya
nyumba zao kuezuliwa mapaa na upepo uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Wakazi wa maeneo ya Kazima ringini,Kilimani
na Kaparangao ambao wamekumbwa na adha hiyo jana na wamesema nyumba zao
zimeharibiwa kabisa na kwamba sasa wanalazimika kulala nje.
Aidha wananchi hao wamesema licha ya
viongozi mbalimbali kufika katika maeneo hayo yaliyokumbwa na majanga akiwemo
mkuu wa wilaya na viongozi wengine hakuna msaada wowote walioupata.
Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa wa Kazima
Ringini Dionisi Clement amesema serikali lazima ichukue hatua za haraka
kuwasaidia wananchi hao.
Mwaka uliopita maafa kama hayo
yalitokea maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au
P5Tanzania Limited Group
Comments