KAMPUNI YA MAFUTA YA GPB YAKABIDHI MRADI WA MAJI KWA MANISPAA YA MPANDA BURE



Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Meya Manispaa ya Mpanda Philipo Mbogo
KAMPUNI ya mafuta ya GPB iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imekabidhi mradi wa maji bure kwa wakazi wa Mtaa wa Majengo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Mpanda Wilium Mbogo akizindua mradi wa maji ya bure unao fadhiriwa na kampuni la GBP linalojihusisha na uuzaji wa mafuta ya Petrol.
Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika kituo cha GBP kilichopo kata ya Majengo mjini Mpanda amewataka wakazi wa eneo hilo kuutumia mradi huo vizuri ili udumu zaidi.
Kwa upande wa Meneja wa Kampuni la GBP katika kituo hicho amesema kampuni hilo limeamua kutoa huduma ya maji kutokana na kuona adha ya maji inavyo wakabili wakazi wa eneo hilo.
Miongoni wa wananchi walio jitokeza katika hafla hiyo wamesema mradi huo ni ukombozi kwa akina mama na familia kwa ujumla.
Mradi huo unatoa zaidi ya lita lakimoja kwa siku ambapo utawanufaisha wakazi wa kata ya majengo na maeneo jirani.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA