DC TANGANYIKA: HATUKUJUA KAMA WANANCHI WANA SILAHA ZA KUPAMBANA NA ASKARI
MKUU wa wilaya ya Tanganyika Salehe
Mbwana Mhando,amesema mwananchi aliyepigwa risasi na askari na kufariki dunia
akiwa katika Hospitali ya Wilaya Mpanda,alipigwa risasi wakati wa majibizano ya
risasi kati ya wananchi na askari.
Mkuu wa Wilaya akizungumza na Mpanda
Radio amesema majibizano kati ya askari na wananchi hao wa eneo la Mnyamasi
linalodaiwa kuwa ni sehemu ya msitu wa hifadhi lililotekea Jumamaosi Oktoba 7 mwaka huu.
Licha ya
kuwa mtu aliyefariki alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda,
Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dkt.Theopista Elisa jana amesema hawezi
kusema ikiwa aliyefariki pamoja na wengine wane walilazwa katika Hosiptali hiyo
wanatokana na sakat hilo.
Kwa mjibu
wa mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyamasi Bw.Magosha Mtoveka amesema tukio hilo
ambalo lilianza juzi na kuendelea mpaka jana pamoja na askari hao wa maliasili
kupiga ovyo risasi za moto pia vyakula na mali nyingine inaelezwa zimechomewa
ndani ya nyumba zao.
Awali
imedaiwa askari walifika kijijini hapo na kuanza kuwafurusha wakazi wa eneo
hilo kwa kutumia nguvu na silaha za moto kwa madai kuwa wamevamia hifadhi ya
msitu wa Mnyamasi ambapo watu saba wanatajwa kurehiwaa.
Suala
hilo linaleta hali ya wasiwasi kwa kuwa Mtu yeyote aliyejeruhiwa ili apatiwe
matibabu lazima majeruhi apatiwe fomu namba tatu (PF3) kutoka polisi inayoeleza
tukio lililompata ambapo watu wanahoji iweje mpaka jana Mganga ashindwe
kubainisha chanzo kilichopelekea watu hao kufikishwa kutibiwa katika hospitali
hiyo.
Kwa mjibu
wa sheria za Tanzania Askari haruhusiwi kutumia risasi za moto kumpiga
mwananchi ambapo matukio mengine kama hayo ya watu kupoteza maisha yamekuwa
yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments