WANAFUNZI 258 MKOANI KATAVI WAKATIZWA MASOMO,RC KATAVI ACHARUKA KWA WANAOWAPA MIMBA



Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Aliyeko katikati katika picha ni RC mkoani Katavi Meja Jeneral Raphael Muhuga
SERIKALI mkoani Katavi imesema itawachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kuwapa mimba au kushiriki mapenzi na wanafunzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ktavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga wakati wa uzinduzi wa kongamano la kujadili mimba za utotoni Mkoani Katavi baada ya Mkoa wa Katavi kutajwa kuwa mkoa namba moja kwa Mimba za utotoni kwa asilimia 45 katika mikoa ya Tanzania Bara.
Muhuga amesema katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 jumla ya wanafunzi 258 wa shule za msingi na sekondari walikatizwa masomo yao kutokana na kupata mimba.
Hivi karibuni Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS Umeutaja Mkoa wa Katavi kuwa kinara wa mimba za Utotoni kwa asilimia 45 ukifuatiwa na Mkoa wa Tabora kwa asilimia 43 ambapo Meneja wa Takwimu kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS Mkoani Katavi Bw.Gideon Mokiwa Amezitaja sababu zinazoweza kupelekea mimba za utotoni kuwa ni pamoja wazazi kuwa na tama ya mali pamoja na kutotambua umuhimu wa mwanamke kupata elimu.
Katika maadhimisho hayo yanayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka,Kaulimbiyu kwa mwaka huu inasema’’Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,tokomeza mimba za utotoni tufikie uchumi wa viwanda’’
Wakati maadhimisho hayo yakiadhimishwa kitaifa Wilayani Tarime Mkoani Mara,katika mkoa wa Katavi yanaadhimishwa katika viwanja vya shule ya Msingi Kashaulili katika Manispaa ya Mpanda
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA